MAWAZO JUU YA MAWAZO, DIAMOND PLATINUM
asubuh ya jumatatu tarehe 9, mwimbaji DIAMOND alifikishwa katika MAHAKAMA ya mwanzo mjini Iringa, kwa kosa la kumpiga mwandishi wa habari na kumvunjia vifaa vyake wiki iliyopita. baada ya kupandishwa leo, mahakama imeamuru msanii huyo kwenda jela miezi sita yeye na wenzake au kulipa faini ya elfu 80 (elfu 50 ya mahakama na 30 ya mlalamikaji) kila mmoja kitendo ambacho kimemkasirisha sana mlalamikaji ambae ndio mwandishi wa habari Francis Godwin. Godwin amesema “sijaridhika na hukumu iliyotolewa pamoja na utaratibu mzima wa uendeshaji wa kesi hiyo, ambapo kwa mara ya kwanza ndio niliona mtuhumiwa akiletwa mahakamani na gari aina ya GX 100, na kingine kilichonishangaza ni kwamba maelezo niliyoyatoa mwanzoni polisi, YAMECHAKACHULIWA na yameletwa mengine na hayajasainiwa” niko na mwanasheria wangu, na tayari nimeshafanya uamuzi wa KUKATA RUFAA katika MAHAKAMA ya juu, eti nashangaa DIMOND amekiri mwenyewe mahakamani kunipiga na kunidhalilisha alafu mahakama imemuamuru anilipe shilingi elfu 30, sasa kama kudhalilishwa ni shilingi elf30 si ningekubali basi mwanzoni wakati DIAMOND aliponitumia shilingi milioni 1.7 ili tumalizane nikakataa?” – Godwin kwa kumalizia, mwandishi huyo amesema “HUKUMU HII ni kama HUKUMU YA KICHINA, na nitaendelea mbele sikati tamaa, kesi naiendeleza”bado DIAMOND hajawa tayari kuizungumzia hii ishu, lakini ameahidi kuzungumza na millardayo.com EXCLUSIVE so time yoyote mzigo nitauweka hapa.
Tuesday, January 10, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment